WOKOVU MKUU
Barua ya Paulo kwa Warumi ni moja wapo ya vitabu muhimu sana katika Bibilia nzima. Umaalum wa kitabu hiki unatokana na uwazi, wepesi na ujumla unaotumia kueleza habari za wokovu wa neema. Wanavyuoni wengi wamehoji kuwa katika barua hii peke yake kunapatikana fundisho lote la Bibilia juu ya mpango na utekelezaji wa wokovu wa Mungu…