Barua ya Paulo kwa Warumi ni moja wapo ya vitabu muhimu sana katika Bibilia nzima. Umaalum wa kitabu hiki unatokana na uwazi, wepesi na ujumla unaotumia kueleza habari za wokovu wa neema. Wanavyuoni wengi wamehoji kuwa katika barua hii peke yake kunapatikana fundisho lote la Bibilia juu ya mpango na utekelezaji wa wokovu wa Mungu kwa wanadamu wenye dhambi. Wengine vile vile wamedai kuwa katika waraka huu mtume ametufundisha tosha jinsi gani ya kuishi maisha ya Kikristo baada ya kupokea imani iletayo wokovu.

MY CONVERSION TESTIMONY  – Wisdom Media Outreach

Umuhimu wa barua hii inajitokeza haswa ukisoma maoni ya mibabe wa imani ya Kikristo katika historia ya kanisa juu ya barua hii. Marehemu R.C Sproul aliwahi kusema kuwa kama angelazimika kuchagua mstari mmoja tu katika Bibilia nzima, wala asipewe fursa ya kuwa na mistari ya ziada kando na hilo moja, angechagua Mwanzo 15:6. Sababu aliyotoa gwiji huyu ni kuwa katika huo mstari mmoja wa Bibilia anaona mukhtasari wa ujumbe wote wa wokovu. Ni kwa sababu kama hiyo pia alisema angepewa fursa ya kitabu kimoja tu katika Bibilia nzima, angechagua kitabu hiki cha Warumi.

Mungu amependezwa katika historia ya kanisa kuitumia kitabu kuwaokoa watu wengi tajika. Yule mkereketwa wa imani ya maandiko Aurelius Augustine alipata kuokoka kwa kusoma kitabu hiki. Vivyo hivyo pia na Martin Luther aliyeongoza mageuzi ya Kiprotestanti.

 vichache vilivyoandikwa kwa malengo maalum ya kuleta fundisho kabambe na maridhawa ya Injili iletayo wokovu. Barua hii tofauti na zingine kama Wakorintho, Wathesalonike, Wakolosai na nyaraka nyingine kama hizo, haijaandikwa kwa malengo ya kutatua shida zilizokumba kanisa. Malengo ya mtume katika waraka huu ni kuweka wazi paruwanja imani yake katika Injili ya Kristo Yesu

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *